KOCHA wa Arsenal ya Arsene Wenger amesema kwamba hivi sasa anahitaji kufanya mageuzi katika kikosi chake.
Wenger aliyasema hayo wakati akizungumza na gazeti moja la nchini humo kuwa amepanga kufanya hivyo baada ya kugundua baadhi ya kasoro.
Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha timu yake inabadilika na kucheza katika kiwango cha hali ya juu mwanzoni mwa mwaka ujao.
"Nataka kubadili mfumo na washambuliaji wangu wasipoteze nafasi ya kupachika mabao, tumekuwa tunapoteza nafasi nyingi," alisema.
Tayari kocha huyo ameanza kuwafuatilia baadhi ya wachezaji akiwamo Kingsley Coman, ili kuongeza nguvu katika kikosi chake.
Comments
Post a Comment