Mohamed Elneny            anatarajiwa kufanya vipimo vya afya Jumanne hii huko Paris            Ufaransa kuelekea usajili wa kujiunga na Arsenal.
        Kiungo huyo wa            Basle atatua Arsenal kwa dili la pauni milioni 7.4 lakini            atapaswa kwanza kusubiri kukamilika kwa hati yake ya kufanya            kazi Uingereza kabla usajili huo haujatangazwa rasmi.
        Mohamed Elneny            mwenye umri wa miaka 23 alirejea Switzerland siku ya mkesha wa Christmas  akitokea Misri kwenye mapumziko wakati            klabu hizo mbili zikiwa kwenye mazungumzo.
        Mchezaji wa            kimataifa wa Misri aliyeichezea nchi yake mechi 36,            anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu Arsenal.
        Kocha wa Arsenal            Arsene Wenger amedhamiria kufanya usajili katika dirisha dogo            ili kuziba mapengo ya kikosi chake kilichojaa majeruhi ili            kuhakikisha timu yake inakaa kwenye mazingira mazuri ya            kupigania taji la Premier League.
        Kiungo wa Basle               Mohamed Elneny anategemewa kufanya vipimo vya afya Jumanne              Arsenal
        Mohamed Elneny (kulia) anatarajiwa kusaini mkataba wa              miaka minne na nusu Arsenal
          
Comments
Post a Comment