Arsenal imedhihirisha kuwa safari hii haitaki kuwa msindikizaji baada ya kuichapa Manchester City 2-1 katika mchezo wa Premier League uliochezwa Jumatatu usiku kwenye uwanja wa Emirates.
Ikitandaza soka la kutakata, Arsenal ikafunga magoli yake mawili katika kipindi cha kwanza kupitia kwa Theo Walcott dakika ya 33 na Olivier Giroud dakika ya 45.
Kwa ushindi huo, Arsenal inayoshika nafasi ya pili kwa kujikusanyia pointi 36, imepunguza pengo la pointi kati yake na vinara Leicester City yenye pointi 38.
Bao pekee la Manchester City liliwekwa kimiani na kiungo Yaya Toure katika dakika ya 82.
Mesut Ozil ndiye aliyetia fora kwa kutengeneza magoli yote mawili ya Arsenal, hatua inayomfanya awe mpishi wa magoli 14 katika mechi 10 zilizopita.
Arsenal (4-2-3-1): Cech; Bellerin, Mertesacker, Koscielny, Monreal; Ramsey, Flamini; Walcott (Chambers 88), Ozil (Oxlade-Chamberlain 76), Campbell (Gibbs 70); Giroud
Manchester City (4-3-2-1): Hart; Sagna, Otamendi, Mangala, Kolarov; Fernandinho, Toure, Delph (Sterling 46); De Bruyne, Silva (Navas 73); Aguero (Bony 63)
Theo Walcott akiifungia Arsena bao la kwanza kufuatia pasi ya kichwa ya Mesut Ozil
Walcott akiwapa saluti mashabiki
Olivier Giroud anafunga bao la pili mbele ya beki wa Manchester City Nicolas Otamendi
Kitendo bila kukosea, Giroud anamchambua kipa Joe Hart
Giroud mwenye umri wa miaka 29 anashangilia bao lake
Comments
Post a Comment