WASHIKA mitutu wa London, Arsenal, wameapa kula sahani moja na timu zinazomwania straika wa timu ya Napoli ya Italia, Gonzalo Higuain.
Taarifa za masuala ya usajili ndani ya Arsenal zinasema kuwa, Gonzalo anapewa nafasi kubwa ya kutua Emirates katika usajili wa mwezi Januari, mwakani.
Wenger amebainisha kuwa kipaumbele chake kwa sasa ni kuimarisha kikosi kwa kumpata mlinzi wa kati, mlinda mlango na mshambuliaji.
Gonzalo pia anawaniwa na timu mbalimbali za England, ikiwamo Manchester United na Chelsea, lakini Wenger anatajwa kuwa anaamini klabu yake itapambana kwa ajili ya kunasa saini ya mshambuliaji huyo.
Comments
Post a Comment