Zlatan Ibrahimovic ameifungia Sweden magoli mawili katika mchezo wa kufuzu Euro 2016 dhidi ya Denmark huku mechi hiyo ya vuta nikuvute ikimalizika kwa sare ya 2-2.
Sare hiyo inafanya Sweden ipate tiketi ya kwenda Euro 2016 kwa jumla bao 4-3 kufuatia ushindi wake wa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza.
Denmark ikiwa nyumbani ililazimika kupambana baada ya kuwa nyuma kwa bao 2-0 lakini sare ya 2-2 bado haikuwasaidia kwenda kwenye fainali za Euro 2016.
Zlatan Ibrahimovic akipiga magoti kushukuru Mungu
Ibrahimovic anafunga kwa free-kick kipindi cha pili ba kuihakikishia Sweden tiketi ya Euro 2016 kiangazi kijacho
Mshambuliaji huyo wa Paris Saint-Germain akifunga bao maridadi
Ibrahimovic akitazama mpira wake ukielekea wavuni
Comments
Post a Comment