ZIDANE ASEMA KWA SASA HANA NJOZI YA KUFUNDISHA REAL MADRID



ZIDANE ASEMA KWA SASA HANA NJOZI YA KUFUNDISHA REAL MADRID
Zinedine Zidane has            revealed that he is not looking to replace Rafa Benitez in            charge of Real Madrid this term
NYOTA wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Zinedine Zidane, amesema huu sio muda sahihi wa yeye kuifundisha klabu yake hiyo ya zamani.

Baada ya Madrid kupokea kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya watani wao Barcelona kwenye mchezo wa El Clasico ambao ulipigwa kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, kuna habari zinasema kuwa, kocha wa klabu hiyo, Rafael Benitez ana uwezekano wa kufukuzwa kazi.

Kutokana na hali hiyo, Zidane ambaye anaifundisha timu B ya klabu hiyo (Castilla), ameonekana kuwa miongoni mwa makocha ambao wanafikiriwa kuchukua nafasi ya Benitez, lakini mwenyewe amesema kuwa hayupo tayari kwa sasa.

"Kwa sasa mimi ni kocha wa Castilla na Benitez ni kocha wa kikosi cha kwanza, najisikia kuwa na amani katika nafasi niliyonayo.


"Ni mapema mno kusema naweza kuwa kocha wa kikosi cha kwanza, huu sio muda sahihi kwangu kufundisha timu hiyo, bado nitaendelea kuwa katika kikosi hiki na kikosi cha kwanza atakuwa Benitez," alisema Zidane. 


Comments