ZENIT ST PETERSBURG YAITUNGUA VALENCIA 2-0 NA KUWEKA HISTORIA YA AINA YAKE CHAMPIONS LEAGUE ...Lyon yakalishwa 2-1 na KAA Gent
Zenit St Petersburg imejihakikishia nafasi ya kwanza kwenye kundi H katika michuano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuifunga Valencia 2-0 huo ukiwa ni ushindi wao wa tano mfululizo.
Oleg Shatov aliwafungia wenyeji bao la kwanza dakika ya 15 kabla ya Artem Dzyuba kuihakikishia ushindi Zenit kwa bao la dakika ya 74.
Ukiwa umesalia mchezo mmoja kwa kila timu, Zenit inajihakikishia kumaliza ya kwanza ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo katika historia yake ya Champions League hatua ya makundi.
Katika mchezo mwingine wa kundi H Lyon ilikubali kipigo cha bao 2-1 kutoka kwa KAA Gent.
Artem Dzyuba (kulia) akishangilia na Danny(kushoto) wa Zenit baada ya kufunga kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Valencia
Zenit na Valencia walicheza kwenye umande mkubwa huku barafu likitanda kando ya dimba
Zenit inaongoza Kundi H ikiwa imeshinda mechi zake zote tano ilizocheza katika hatua ya makundi Champions League
Comments
Post a Comment