VAN GAAL: ROONEY HACHEZI KWASABABU TU NI NAHODHA


VAN GAAL: ROONEY HACHEZI KWASABABU TU NI NAHODHA

Wayne Rooney UEFA

Kocha Louis Van Gaal anasema hamchezeshi Wayne Rooney kwasababu tu ni nahodha wa timu bali ni umuhimu wake kikosini ikiwa ni pamoja na kusaidia timu kwa kiasi kikubwa achilia mbali ukame wa kufunga magoli unaomkabiri nahodha wake.

Kuelekea katika mchezo wa leo jioni dhidi ya Leicester City wanaoongoza ligi kuu nchini England hivi sasa, Van Gaal amemtaka Wayne Rooney kuibuka shujaa juu ya mshambuliaji aliyekatika fomu nzuri hivi sasa Jamie Vardy wa Leicester ambaye pia ndio kinara wa mabao huku Rooney akiwa amefunga mara mbili tu tangu kuanza kwa msimu huku wa ligi kuu soka nchini England.

Van Gaal anasema kuwa kama Rooney angekua hana mchango chanya kwa timu yake, asingekua na nafasi ya kuanza kikosini lakini akasisitiza kuwa achilia mbali kufunga magoli, lakini Rooney amekua na mchango mkubwa kwenye time na hivyo hapangwi kwa sababu ya kitambaa.

Kocha huyo amesisitiza kuwa amekua akipanga timu kutokana na 'game plan' na hivyo Martial na Rooney wamekua wakibadilishana nani akae juu zaidi ama vinginevyo.

Leicester leo wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri za ushindi wa bao 5-3 dhidi ya Manchester United msimu uliopita katika uwanja wao wa nyumbani, huku kocha Louis Van Gaal akisisitiza kuwa mshambuliaji wao Jamie Vardy ni mgumu zaidi kumzuia asifunge.



Comments