VAN GAAL AKIRI KUWANIA KUMSAJILI CRISTIANO RONALDO MSIMU UJAO



VAN GAAL AKIRI KUWANIA KUMSAJILI CRISTIANO RONALDO MSIMU UJAO
Kocha wa Manchester United  Louis van Gaal ameweka wazi kuwa atapambana kumsajili Cristiano Ronaldo iwapo mchezaji huyo ataamua kuondoka Real Madrid.

Ronaldo, 30, kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na kurejea Old Trafford hususan ndani ya miaka miwili iliyopita na sasa inaaminika kuwa ataruhusiwa kuondoka Bernabeu kiangazi kijacho huku kocha  Rafa Benitez akitarajiwa kuijenga timu kupitia Gareth Bale.

Mwaka 2o13 United ilijaribu kumsajili bila mafanikio mshindi huyo wa tuzo tatu za mchezaji bora wa dunia.

Lakini safari hii huku Louis van Gaal akilalamikia uhaba wa wachezaji wa pembeni kwenye kikosi chake, Mholanzi huyo amethibitisha kuwa Ronaldo yuko kwenye kikosi akili yake.

"Anacheza pembeni, ana kasi na anafunga magoli. Sidhani kama kuna kocha duniani ambaye asingependa kuwa nae," alisema kocha huyo wa Manchester United.

"Kwa hakika tunamfuatilia. Tunaangalia wachezaji wote, sio Ronaldo tu, lakini wachezaji wa aina hii ni ngumu kuwanasa. Wacha tusubiri na kuweka matumaini."
Bosi wa Manchester United Louis van Gaal ameweka wazi kuwa angependa kumsajili Cristiano Ronaldo msimu ujao
Ronaldo (left) looks set to                  leave the Santiago Bernabeu following the arrival of                  manager Rafa Benitez (right)
Ronaldo (kushoto) akiwa na Rafa Benitez 
Benitez has plans to build                  his Real Madrid side around Welsh star Gareth Bale                  (left), rather than Ronaldo
Benitez amedhamiria kuijenga Real Madrid kupitia kwa Gareth Bale (kushoto) kuliko Ronaldo



Comments