VALENCIA YA HISPANIA YAMPIGIA HESABU DARREN FLETCHER



VALENCIA YA HISPANIA YAMPIGIA HESABU DARREN FLETCHER

KLABU ya Valencia ya Hispania haisikii lolote kwa kiungo mkabaji wa zamani wa Manchester United, Darren Fletcher na sasa wamepanga kupiga hodi kwa West Brom kukamilisha dili la kumnyakua jumla.

Fleatcher mwenye umri wa miaka 31, amekuwa katika kiwango cha hali ya juu kwa sasa tangu atue West Brom akitokea kwa Mashetani Wekundu wa Manchester United.

Valencia wanaamini kuwa, Fleatcher mwanandinga sahihi katika kikosi chao kinachopigana kufa na kupona katika LaLiga.

Hata hivyo Darren anajikuta hana nafasi katika kikosi cha kwanza, akiwa na kumbukumbu ya kucheza mechi tatu tu tangu kuanza kwa Ligi ya msimu huu.


Comments