UHOLANZI YAIBUKIA KWA WALES


UHOLANZI YAIBUKIA KWA WALES

Uholanzi yaibuka

Uholanzi wameibuka na kuikandamiza Wales kwa bao 3-2 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao Wales waliutumia kwa maandalizi ya kuelekea michuano ya Euro mwaka 2016.

Bas Dost alianza kufunga goli la kuongoza kwa upande wa Uholanzi lakini Wales wakasawazisha goli hilo kupitia kwa Joe Ledley. Arjen Robben akapachika bao la pili lakini Emyr Huws akasawazisha kwa kichwa na kufanya sare ya magoli 2-2.

Nahodha wa Uholanzi Arjen Robben akaamua mchezo huo kwa kupiga goli la tatu na la ushindi kwa Uholanzi. Wales wamepoteza michezo yao yote saba ambayo wamekutana na Uholanzi huku wakiubali kuruhusu jumla ya magoli 21 wakati wao wakiwa wamefunga matatu tu.

Uholanzi yaibuka 1

Licha ya kupoteza mchezo huo, Wales wameonesha kiwango kizuri mbele ya Uholanzi ambao wameshindwa kufuzu kwa michuano ya mataifa ya Ulaya (Euro 2016).

Uholanzi yaibuka 2



Comments