UGANDA YAISAMBARATISHA TOGO NA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA 2018



Wachezaji wa Uganda wakipongezana baada ya kufunga moja              ya magoli yao (Picha kwa hisani ya Kawowo Sports)
Wachezaji wa Uganda wakipongezana baada ya kufunga moja ya magoli yao (Picha kwa hisani ya Kawowo Sports)

Uganga imekuwa timu ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki kuingia kwenye hatua ya makundi kutafuta nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga timu ya Togo kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela, Uganga.

Bao la kwanza lilifungwa na Geoffrey Massa dakika ya tatu kipindi cha kwanza huku Miya Farouk akifunga bao la pili na la tatu katika dakika za 28 na 45.

Uganda wamefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4-0 kufuatia ushindi waliopata ugenini (Togo) wa goli 1-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Alhamisi iliyopita.

Ushindi huo wa Uganda ni kama wamelipa kisasi kwani kwenye mechi za kufuzu kwa ajili ya fainali za mataifa ya Afrika miaka mitatu iliyopita Togo iliifunga Uganda kwenye mechi zote nyumbani na ugenini.



Comments