TONNY ADAM ASEMA MESUT OZIL NI BONGE LA MCHEZAJI ILA AMEINGIA ARSENAL KIPINDI KIGUMU



TONNY ADAM ASEMA MESUT OZIL NI BONGE LA MCHEZAJI ILA AMEINGIA ARSENAL KIPINDI KIGUMU
Arsenal midfielder Mesut Ozil claims extra shooting            practice is the reason behind his attacking improvement
MASHABIKI wa klabu ya Arsenal wameonywa kuacha kuwasakama wachezaji wao, hasa kiungo Mesut Ozil (pichani juu).
Onyo hilo limetolewa na nahodha wa zamani wa klabu hiyo, Tonny Adam ambaye amesema mashabiki wanamfanya mchezaji huyo kucheza kwa shinikizo.
Alisema kuwa, Ozil aliyeng'ara katika mchezo wa Arsenal dhidi ya mahasimu wao wa jiji la London, Tottenham Hotspurs wikiendi iliyopita, ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi.
Alisema, amemfuatilia mchezaji huyo na kubaini ana uwezo mkubwa isipokuwa amekuja wakati klabu hiyo ikiwa katika kipindi kigumu cha kukosa mataji.
"Nadhani mashabiki wa Arsenal wanapaswa kuwaacha wachezaji wafanye kazi yao, shutuma zao nzito zinawapa shinikizo na kuwafanya waharibu zaidi," alisema Adam.
"Siwezi kusema kuwa Ozil ameisaidia Arsenal kwa mechi dhidi ya Tottenham, bali kwenye mechi hiyo ameonyesha thamani yake halisi kuwa ni mchezaji muhimu anayefanya vizuri kila mara, anapaswa kuungwa mkono na wote," alisema Adam.
Katika mchezo huo, Ozil ndie aliyefanya kazi kubwa kabla ya kutoa krosi kwa Kieran Gibbs aliyewafungia Arsenal bao la kusawazisha na kuambulia pointi moja baada ya kutoka sare ya bao 1-1.



Comments