TFF YATANGAZA TENDA KUWEZESHA TIKETI ZA ELEKTRIONIKI



TFF YATANGAZA TENDA KUWEZESHA TIKETI ZA ELEKTRIONIKI

KATIKA kile inachoonekana na kuteswa na jinamizi la kufeli kwa tiketi za elektroniki, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetangaza tenda.

TFF kwa kushirikiana na mzabuni wa tenda hiyo ya elektroniki, benki ya CRDB, wametangaza tenda ya kusaka mshauri wa mfumo wa elektroniki.

Jukumu la mshauri huyo ni kupitia na kuwashauri namna ya kuondoa mapungufu yaliyopo katika mfumo wa uuzaji tiketi wa elektroniki katika michezo ya igi Kuu ya Vodacom Tanzania.

TFF imetangaza tenda hiyo, ili kumpata mshauri wa mfumo huo wa tiketi za elektroniki ambao ulisimamishwa na serikali Aprili, mwaka huu.

Kusimamishwa kwa matumizi ya tiketi za elektroniki kulitokana na kupungua kwa mapato tofauti na ilivyotarajiwa pamoja na kusababisha usumbufu mkubwa, ikiwamo mashine kugoma wakati mashabiki wameshanunua tiketi jambo lililosababisha mara kadha kutokea vurugu.

Katika tarifa yake, TFF imesema maombi ya tenda yawasilishwe katika ofisi ya katibu Mkuu wa TFF iliyopo uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi sa 10:00 jioni, siku za kazi, Jumatatu hadi Ijumaa.

Gharama ya fomu ya kuombea tenda hiyo ni sh. 100,000 na mwisho wa kuwasilisha maombi ni Desemba 17, mwaka huu.


Comments