STEVEN GERRARD KUVAA TENA UZI MWEKUNDU WA LIVERPOOL MWEZI JANUARI



STEVEN GERRARD KUVAA TENA UZI MWEKUNDU WA LIVERPOOL MWEZI JANUARI
The 35-year-old LA            Galaxy midfielder said Klopp has lifted the whole club since            joining in October
NYOTA wa zamani wa  Liverpool ambaye alikuwa nahodha wa klabu hiyo, Steven Gerrard, anatarajiwa kuivaa tena jezi ya klabu hiyo Januari, mwakani.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya LA Galax ambayo inashiriki Ligi Kuu nchini Marekani, atavaa tena jezi ya Liverpool katika mchezo ambao utawakutanisha nyota wa zamani wa klabu hiyo dhidi ya klabu ya nchini Australia.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 35, kwa sasa yupo jijini Liverpool kwa mapumziko, lakini Januari mwakani wachezaji wa zamani wa klabu hiyo kama vile Jamie Carragher, Dietmar Hamann na John Riise, watavaa uzi wa klabu hiyo kwa ajili ya mchezo wa kirafiki nchini Australia.

"Itakuwa ni siku muhimu kwangu kuvaa tena jezi ya Liverpool nikiwa na wachezaji wenzangu wa zamani.

"Kikosi hicho kitaonyesha ubora wake lakini furaha yangu ni kukutana na nyota wenzangu tukiitumikia klabu hiyo.

"Ninaamini bado tuna mashabiki wengi na ninawakumbuka kutokana na kile ambacho walikuwa wanakifanya, mchezo huo utakuwa wa hisia kali kwangu kutokana na mashabiki hao," alisema Gerrard.

Nyota huyo aliitumikia klabu iyo kwa miaka 17, tangu alipojiunga akiwa na umri mdogo mwaka 1998, ambapo alicheza jumla ya michezo 504 na kufanikiwa kuifungia klabu hiyo mabao 120.


Comments