Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amesema anafanya kila awezalo ili awe fiti kwa mchezo wa Premier League Jumamosi hii dhidi ya Liverpool.
Aguero amekuwa nje ya dimba kwa wiki sita kufuatia maumivu ya msuli aliyoyapata Oktoba 9 wakati alipokuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Argentina dhidi ya Ecuador.
Mshambuliaji huyo bingwa wa kuzifumania nyavu hakuichezea Manchester City tangu ilipomenyana na Newcastle ambapo yeye mwenyewe alisukumiza wavuni mabao matano ndani ya dakika 20.
Aguero ameanza mazoezi kamili wiki hii na anaonekana kupania kushiriki mpambano wa Jumamosi kwenye dimba la Etihad Stadium.
"Natumai nitaweza kucheza mchezo huu," Aguero ameiambia tovuti ya klabu (www.mcfc.co.uk). "Ninafanya kila niwezalo kwa nguvu zangu zote kuwa fiti kwa mchezo wa Jumamosi."
Sergio Aguero akishangilia moja ya mabao yake
Comments
Post a Comment