SANCHEZ, OZIL, KUPEWA MIKATABA MIREFU ARSENAL



SANCHEZ, OZIL, KUPEWA MIKATABA MIREFU ARSENAL

Sanchez mkataba mpya

Klabu ya Arsenal ya England inajiandaa kumpa mkataba mpya mchezaji wake Alexis Sanchez wa miaka mitano kabla ya kumpa dili hilo tena mjerumani Mesut Ozil ambao wote wamebakiza misimu miwili na nusu kila mmoja huku klabu ikihofia kufanya nao mazungumzo katika miaka miwili ya mwisho.

Alexis Sanchez ambaye analipwa pauni 130,000 kwa wiki hivi sasa anatarajiwa kuongezewa hadi kufikia mshahara wa pauni 155,000 kwa wiki kama atasaini mkataba huo mpya wa miaka mitano.

Tayari mazungumzo baina ya maafisa wa klabu na wawakilishi wa Sanchez yanaendelea na taarifa zinasema yanaendelea vizuri na kwamba ni taarifa nzuri kwa kocha Arsene Wenger ambaye amekua akimtegemea zaidi mchezaji huyo tangu atue Arsenal akitokea Barcelona.

Wakati huo huo Arsenal pia inajiweka sawa kumfunga pia mjerumani Mesut Ozil ambaye naye amebakiza msimu miwili na nusu katika mkataba wake wa sasa ambao ndio anaongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa wa pauni 140,000 huku klabu ikitaraji kuendelea kufanya mchezaji anayelipwa zaidi klabuni hapo hata atakapo saini mkataba mpya wa miaka mitano.

Mesut Ozil mkataba mpya

Ozil na Alexis Sanchez wamekua ndio nguzo imara ya Arsenal tangu kutua klabuni hapo na wameisaidia klabu huyo kutwaa mataji ya FA katika misimu miwili mfululizo mwaka juzi na mwaka jana.



Comments