ROONEY AWAZIMA MIDOMO WANAOMBEZA, AING’ARISHA ENGLAND MBELE YA FRANCE


ROONEY AWAZIMA MIDOMO WANAOMBEZA, AING'ARISHA ENGLAND MBELE YA FRANCE

Rooney areajea

Wazungu wana usemi usemao, "Class is permanent, form is temporary" wakimaanisha uwezo na kipaji ni kitu kikubwa zaidi ya kiwango 'fomu' ambayo huja na kupotea.

Usemi huo ulithibitika jana usiku England wakicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa, katika usiku wa kukumbukwa Wembley baada ya mataifa hayo makubwa mawili kuonesha mshikamano wao katika wakati huu mgumu ambapo magaidi wanavamia katika mataifa ya Ulaya.

Wayne Rooney tofauti na matarajio ya wengi wanaombeza siku za hivi karibuni, alikua katika fomu ya hali ya juu sana akitoa pasi ya goli la kwanza kwa kiungo anayechipukia Dele Alli wa Tottenham Hotspur, kabla ya yeye kuunganisha mpira uliopigwa na winga Rahem Sterling na kuiandikia England goli la pili na kufanya matokeo kuwa 2-0.

Wachambuzi nchini England wameanza kunyoosheana vidole huku wengi wakisema walimuhukumu Rooney mapema na kusahau bado mchezaji huyo alikua anapitia mapito kama binadamu na mwanasoka mwingine yeyote duniani.

Baada ya mchezo huo Rooney na Hugo Lloris wa Ufaransa walisema mechi hiyo ilikua muhimu kwao kuungana na kuonesha wako kinyume na vitendo vya kigaidi vinavyoshamiri hivi sasa.



Comments