RIO FERDINAND HAIKUBALI KABISA 'KOMBINESHEN' YA SCHWEINSTEIGER NA MORGAN SCHNEIDERLIN NDANI YA MANCHESTER UNITED
Sentahafu wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand amesema ni wazi kuwa mashabiki wa timu hiyo hawana furaha na mfumo wa kocha Louis van Gaal, lakini akafichua kuwa hilo linachangiwa na kupwaya kwa safu ya kiungo Old Trafford.
Rio Ferdinand anaona bado hakuna uwiano mzuri wa kiungo cha kati na akaenda mbali zaidi kwa kusema safu inayoundwa na Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin inashindwa kuilainisha timu.
Beki huyo anasema kama yeye angekuwa ni mchezaji wa kiungo na akapewa jukumu la kukabiliana na Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin basi asingekuwa na chochote cha kuhofia.
Morgan Schneiderlin mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa alinunuliwa kutoka Southampton majira ya kiangazi kwa kitita cha pauni milioni 25 wakati mshindi wa Kombe la Dunia Bastian Schweinsteiger aliwasili kutoka Bayern Munich kwa pauni milioni 7.
Ferdinand anadai kwa aina ya wachezaji ilionao Manchester United, mbinu za Van Gaal ni sahihi katika kuinasua klabu hiyo kwenye ukame wa mafanikio.
Ferdinand ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka anasema Van Gaal hastahili kupuuzwa
Ferdinand havutiwi na uchezaji wa Bastian Schweinsteiger kwenye safu ya kiungo
Ferdinand anaamini kombineshen ya Schweinstiger na Morgan Schneiderlin haijazaa matunda
Van Gaal (kulia) na Giggs wamesaidia kurejesha United kwenye Champions League
Comments
Post a Comment