Kinyume na anavyohusishwa na Manchester City, lakini kocha Pep Guardiola anapendelea kuinoa Manchester United mara atakapomalizana na Bayern Munich.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na Guardiola, kocha huyo anataka kufundisha Premier Leagua huku Manchester United ikiwa chaguo lake namba moja.
Bayern Munich inatarajia kuwa mwishoni mwa mwaka huu Guardiola ataamua hatma yake juu ya mkataba wake unaomalizaka mwishoni mwa msimu huu.
Manchester City siku zote imekuwa ikiamini kuwa kwa kuwachukua Ferran Soriano kama mtendaji mkuu na Txiki Begiristain kama mkurugenzi wa michezo, kutasaidia kumnasa Guardiola kutokana na uhusiano wao mzuri tangu walipokuwa Barcelona.
Wakala wa Guardiola, Josep Maria Orobit alikuwa England Alhamisi iliyopita na kuzua tetesi kuwa alikwenda kushughulikia dili la kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 kujiunga na Manchester City.
Lakini bado vyanzo vingi vya habari vinasema ni kweli Guardiola anataka kwenda Premier League lakini ni Manchester United na sio Manchester City.
Pep Guardiola angependelea kujiunga na Manchester United
Bayern Munich inataraji Guardiola ataamua hatma yake mwishoni mwa mwaka
Comments
Post a Comment