NEYMAR HASOMEKI BARCELONA ...MAN CITY NA MAN UNITED ZATAJWA KUMVURUGA AKILI



NEYMAR HASOMEKI BARCELONA ...MAN CITY NA MAN UNITED ZATAJWA KUMVURUGA AKILI

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona FC, Neymar hasomeki kabisa kwenye suala linaloitwa msimamo na sasa inadaiwa amepanga kuondoka katika timu hiyo.

Taarifa iliyotolewa na gazeti moja la nchini Hispania, imeeleza kuwa nyota huyo amepanga kuondoka baada ya kutokuwa na  namba ya kudumu hususan kwenye eneo la ushambuliaji wa kati.

Tayari kuna taarifa kuwa, huenda akatua ndani ya kikosi cha timu ya Manchester City kwa ajili ya kuichezea msimu ujuo huku Manchester United nayo pia ikihusishwa katika kukivuruga kichwa cha mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil.




Comments