mwanamichezo Majid Adam Issa Maki afariki dunia


mwanamichezo Majid Adam Issa Maki afariki dunia
Tasnia ya michezo hususani kandanda  imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mwanamichezo mkongwe Majid Adam Issa Maki (pichani) aliyefariki alfajiri ya leo. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Yombo, Dar es salaam na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo saa kumi katika makaburi ya Kisutu.
Marehemu, ambaye ni mtoto wa Mwalimu Adam Issa Maki,  atakumbukwa kama mmoja wa wachezaji mahiri wa klabu ya Sunderland (Simba) na pia mmoja wa waanzilishi wa klabu ya Red star ambako alikuwa team manager.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un



Comments