Licha ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Tottenham, kocha wa Chelsea Jose Mourinho amekimwagia sifa kikosi chake kutokana na kiwango kilichoonesha kwenye mchezo wa leo kikiwa ugenini ambako kiliambulia pointi moja.
Mourinho amesema kiwango kilichooneshwa na timu yake leo kikubwa kuwahi kutokea tangu kuanza kwa msimu huu na anaamini timu yake ilipaswa kupata matokeo mazuri zaidi ya ilioyapata kwenye mchezo huo.
Kocha huyo mwenye mbwembwe za maneno mengi ameongeza kuwa, Chelsea sasa inaanza kurejesha makali yake ya awali huku akiwasifu Hazard na Oscar kwa viwango walivyovionesha kwenye mchezo huo dhidi ya Spurs.
Mourinho amesema timu yake imecheza vizuri hasa katika safu ya ulinzi kwa kufanikiwa kuizuia timu tishio kwa sasa isipate goli lakini hakusita kusema kuwa walitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini hawakufanikiwa kufanya hivyo.
Pia Mourinho amesema anauhakika timu yake itasogea juu baada ya kucheza michezo mitano waliyonayo mwezi December na kuhakikisha timu inasogea kwenye nafasio nzuri zaidi.
Comments
Post a Comment