MOURINHO AMCHIMBA ‘MKWARA’ DIEGO COSTA, AMTAKA ABADILIKE


MOURINHO AMCHIMBA 'MKWARA' DIEGO COSTA, AMTAKA ABADILIKE

Costa

Kocha Jose Mourinho wa Chelsea, ameponda uwezo wa nyota wake Diego Costa kwamba amepoteza makali na kwamba anashindwa kuongoza timu ipasavyo katika safu ya ushambuliaji tofauti na ilivyokua msimu uliopita, huku akimtaka abadilike haraka kama anataka kuwa katika kiwango chake.

Kocha huyo na mchezaji wake walitibuana Jumatano hii katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Maccabi Tel Aviv baada ya Mourinho kutoridhishwa na uchezaji wa mshambuliaji huyo lakini baadae kocha huyo akasema walisuluhisha katika chumba cha kubalishia nguo kwa 'kisses & cuddles'.

Chelsea inakabiliwa na mlima kubwa kesho Jumapili itakapoumana na klabu ya Tottenham Hotspur saa tisa alasiri katika uwanja wa White Hart Lane huku mshambuliaji wa Spurs, Harry Kane akiwa katika chorus ya kufunga karibu katika kila mechi huku Diego Costa akiwa anahangaika.

Wakati huo huo Mourinho amepotezea kauli ya mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Didie Drogba kwamba Chelsea hivi sasa inakosa viongozi katika chumba cha kubadilishia nguo, huku Mourinho akisema kuwa mchezaji wake huyo wa zamani anajaribu kuuza kitabu chake kipya alichokitoa hivi sasa.



Comments