Kiungo mkongwe wa Manchester United Michael Carrick anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda kutokana na kuumia kinachodhaniwa ni Ankle Ligament baada ya kutolewa nje kwa machela katika mchezo kati ya England na Hispania.
Carrick ambaye aliitwa tena kikosini mara baada ya fainali za kombe la dunia mwaka jana, ameanza katika kikosi cha kwanza mara mbili tu kutokana na muda mwingi kuwa majeruhi.
Baada ya kumalizika mchezo huo kwa Spain kushinda bao 2-0 dhidi ya England, kocha wa England Roy Hodgson amesema Carrick anarudi leo nchini England kwa vipimo zaidi lakini akasisitiza kwamba huenda Carrick mwenye miaka 34 hivi sasa akakaa nje kwa muda mrefu.
England sasa inakabiriwa na majeruhi muhimu wa kikosi cha kwanza akiwemo Jordan Henderson, Jack Wilshere na Luke Shaw ambapo pia Theo Walcott na Oxlade Chamberlain nao ni wagonjwa.
Comments
Post a Comment