MESSI MWAMCHE TU, AIONGOZA BARCELONA KUIFUMUA ROMA 6-1 ...BATE Borisov na Bayer Leverkusen zatoshana nguvu
Lionel Messi amedhihirisha kuwa majereha yaliyomweka nje ya dimba kwa wiki kadhaa, hayajapunguza makali yake.
Mshambuliaji huyo ameng'ara sana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma ambapo timu yake ya Barcelona imevuna ushindi wa bao 6-1.
Kama vile hiyo haitoshi, Messi akafunga mara mbili huku Luis Surez nae akifunga mara mbili wakati Gerard Pique na Adriano wakifunga mara moja kila mmoja.
Bao pekee la Roma lilifungwa na Eden Dzeko dakika ya 90, dakika nane baada ya mshambuliaji huyo kupoteza mkwaju wa penalti.
Huo ulikuwa mchezo wa kundi E ambao ulishuhudia pia timu za BATE Borisov na Bayer Leverkusen zikitoshana nguvu kwa sare ya 1-1. Barcelona tayari imefuzu kwenda hatua ya 16 bora.
Lionel Messi akifunga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa
Messi akifanya vitu vyake Nou Camp
Comments
Post a Comment