MESSI AMEICHAGUA CLUB HII YA EPL NA KIASI HIKI CHA MSHAHARA KAMA AKIHAMIA.


MESSI AMEICHAGUA CLUB HII YA EPL NA KIASI HIKI CHA MSHAHARA KAMA AKIHAMIA.

Zimebaki siku 5 kuelekea mechi kubwa ya La Liga ambayo ni maarufu kwa jina la El Clasico wachezaji Messi na Ronaldo wanaandikwa sana.

Habari kutoka gazeti la The Star zinasema kwamba Messi kama akijiunga na club ya yoyote ambayo inayocheza EPL, basi atahitaji kulipwa kiasi cha pound laki 6 kila wiki.

Pia gazeti hilo linaendelea kutoa habari kwamba Messi ameichagua Arsenal dhidi ya Manchester United au Manchester City.

Kuna story zinasema kwamba Messi anaweza kuhama Barcelona kwasababu ya matatizo mengi anayopata kutokana na mambo ya kodi na kesi za mahakamani. Lakini pia kiongozi wa ngazi ya juu ya Barcelona alisema kwamba Messi atacheza Barcelona hadi mwisho wa career yake.



Comments