MEMPHIS DEPAY ASHIKA NAMBA TATU DUNIANI KWA UUZAJI WA JEZI … LIONEL MESSI NAMBA MOJA CRISTIANO RONALDO WA PILI
Licha benchi kuanza kumzoea Manchester United, winga Memphis Depay ni mchezaji wa tatu baada ya Lionel Messi na Cristiano Ronaldo pale linapokuja suala la uuzaji wa jezi.
Mtendaji mkuu wa Manchester United Ed Woodward ametoa takwimu hiyo ya kushangaza huku akifichua kuwa kiungo Bastian Schweinsteiger amepaa kutoka namba 31 hadi namba nne katika orodha ya wanasoka ambao majina yao yanaongoza kwa kuuza jezi ulimwenguni msimu huu.
Bastian Schweinsteiger amekwea ngazi hizo mara baada ya kujiunga na Manchester United akitokea Bayern Munich.
Lionel Messi ndiye mbabe wao akiwa anakamata namba moja huku akifuatiwa na mpinzani wake mkubwa Cristiano Ronaldo.
Memphis Depay ni mmoja wa wanasoka wanaotesa kwa kuuza jezi
Lionel Messi ndio namba moja kwa uuzaji wa jezi
Comments
Post a Comment