MASIKINI DANIEL STURRIDGE..!! AUMIA TENA


MASIKINI DANIEL STURRIDGE..!! AUMIA TENA

Daniel Sturridge

Mshambuliaji Daniel Sturridge wa Liverpool jana alishindwa kucheza katika mchezo wa Uropa ligi kati ya timu yake ya Liverpool na Bordeux ya Ufaransa baada ya kuumia muda mchache kabla ya mechi kuanza.

Sturridge ambaye amefanikiwa kuichezea Liverpool mechi tatu tu tangu kuanza kwa msimu huu, aliumia katika mazoezi na haijajulikana itachukua muda gani, huku kocha Jurgen Klopp akisema hajui nini kinaendelea kwa nyota wake huyo aliyeifungia Liverpool magoli 42 katika michezo 70 aliyoichezea klabu hiyo.

Katika mchezo huo, magoli yaliyofungwa na Christian Benteke na mbrazil Firmino yalitosha kuivusha Liverpool hadi hatua ya 32 bora baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 katika uwanja wa Anfield.

Daniel Sturridge amekua akisumbuliwa na majeruhi mara kwa mara kitu kinachotishia maendeleo yake ya soka pamoja na kuwa na rekodi nzuri ya wastani wa kufunga goli kwa dakika katika historia ya klabu.



Comments