MANCHESTER UNITED YAJICHELEWESHA KUFUZU 16 BORA YA CHAMPIONS LEAGUE …pata matokeo ya mechi zote za Jumatano usiku
Wakati timu kibao zikiwemo Real Madrid, PSG, Barcelona, Bayern Munich, Juventus na FC Zenit, zimejihakikishia nafasi ya kusonga mbele Ligi ya Mabingwa, mambo yamekuwa tofauti kwa Manchester United.
Klabu hiyo ya Old Trafford ilihitaji kujishinda kwenye uwanja wake wa nyumbani dhidi ya PSV Eindhoven ili kuwa na uhakika wa kupenya 16 bora, lakini ikaambulia sare ya 0-0.
United imebaki nafasi ya pili ikiwa na pointi 8 na sasa itakuwa na kibarua kigumu cha kuifunga Wolfsburg inayoongoza kundi B hapo Disemba 8.
Klabu nyingine ya England Manchester City nayo ilijichelewesha baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Juventus ya Italia kwenye mchezo wa kundi D.
Matokeo ya mechi zote za Ligi ya Mabingwa zilizocheza Jumatano usiku ni kama ifuatavyo.
Matokeo ya mechi zote za Ligi ya Mabingwa
Msimamo ulivyo katika makundi A, B, E na F
Msimamo ulivyo katika makundi C, D, G na H
Heka heka kwenye lango la PSV
Comments
Post a Comment