Manchester United ililazimika kutoka nyuma na kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Leicester katika mchezo mkali wa Premier League.
Mshambuliaji tishio wa Leicester Jamie Vardy alikuwa wa kwanza kufunga katika dakika ya 24 na kufanikiwa kuweka rekodi mpya ya kufunga mechi 11 mfululizo.
Kabla ya hapo Jamie Vardy alikuwa akilingana na mshambuliaji wa zamani wa Manchester United aliyekuwa na rekodi ya kufunga katika mechi 1o mfululizo za Premier League.
Kiungo wa zamani wa Bayern Munich aliyejiunga na Manchester United msimu huu, Schweinsteiger alizawazisha sekunde chache kabla ya mapumziko.
Leicester: Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Kante, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy.
Mfungaji: Vardy, 24.
Man Utd: De Gea, McNair, Smalling, Blind, Darmian, Carrick, Schweinsteiger, Young, Mata, Rooney, Martial.
Mfungaji: Schweinsteiger, 45
Jamie Vardy akishangilia bao lake
Darmian akijaribu kumzuia Vardy bila mafanikio
Mshambuliaji wa Leicester Vardy akijipiga kifua kwa furaha baada ya kuweka rekodi mpya ya kupachika mabao Premier League
Vardy akipongezwa na wachezaji wenzake
Kiungo wa Manchester United Bastian Schweinsteiger akiisawazishia timu yake
Schweinsteiger akishangilia baada ya kuisawazsihia United dhidi ya Leicester
Shangwe kwa wachezaji wa Manchester United
Comments
Post a Comment