Ni wakati wa kutunishiana msuli. Southampton inatarajiwa kuizuia Manchester United isimsajili mshambuliaji wao Sadio Mane katika dirisha dogo la usajili la Januari.
Lakini pamoja na hayo, kuna hisia zimetanda Southampton kuwa Mane ataondoka kwenye klabu hiyo mara tu msimu huu utakapomalizika.
Iwe ni Januari au kiangazi kijacho, kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amedhamiria kumsajili winga huyo ambaye alimkosa katika usajili wa kiangazi kilichopita.
Winga wa Southampton Sadio Man anawindwa na Manchester United
Kocha wa United United Louis van Gaal anataka kusajili winga katika dirisha hili usajaji
Comments
Post a Comment