Zikiwa zimebaki siku nne kuelekea mchezo wa mahasimu wakubwa wa soka la Hispania, El Classico inayowakutanisha miamba yasoka Real Madrid na Barcelona, Lionel Messi ameanza mazoezi Jumatatu hii tayari kwa mechi hiyo.
Habari hizi sio za kufurahisha kwa mashabiki wa Real Madrid ambao wasingependa kukutana na Barcelona hii yenye Lionel Messi ndani huku pia Ivan Rakitic naye akitajwa kuwa fit baada ya kupona majeraha yake.
Mchezaji Lionel Messi ambaye alikaa nje ya uwanja, tangu alipoumia mwishoni kwa mwezi September Barcelona ikicheza dhidi ya Las Palma's anatarajiwa kucheza katika mchezo huo utakao pigwa Santiago Bernabeu uwanja wa Real Madrid Jumamosi hii.
Barcelona haikuoekana kuyumba sana baada ya kukosekana kwa nyota huyo, ujio wake ni habari za faraja kwa mashabiki wa Barca na kocha wao Luiz Enrique ambao sasa watakua wanaombea kuona mchezaji huyo anarudia kiwango chake pamoja na kuwa alikua nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili.
Comments
Post a Comment