MACHUPA: UWAZI UNATAKIWA KATIKA SOKA LA KISASA TUSIKARIRI MAJINA, BADO NAIPENDA TIMU YANGU YA TAIFA


MACHUPA: UWAZI UNATAKIWA KATIKA SOKA LA KISASA TUSIKARIRI MAJINA, BADO NAIPENDA TIMU YANGU YA TAIFA
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na timu ya taifa ya              Tanzania 'Taifa Stars'
Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'

Baada ya Stars kupata kipigo cha bao 7-0 dhidi ya Algeria kwenye mchezo wa kusaka nafasi ya kupangwa kwenye makundi ili kuwania nafasi ya kushisiriki michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini Urusi, wadau mbalimbali wa soka wamekuwa na maoni tofauti juu ya matokeo hayo.

Mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Simba SC na timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Athumani Idd Machupa ametoa maoni yake kupitia mtandao wa kijamii akieleza kusikitishwa kwake na matokeo hayo na kushauri nini kifanyike ili kuboresha timu ya taifa.

Machupa ameshauri wachezaji vijana wape nafasi zaidi kuliko wale ambao umri umeenda kwasababu wanashindwa kwenda na kasi ya vijana pamoja na soka la kisasa.

Machupa

"Kessy na Tshabalala wapewe nafasi mabeki wa kati waangaliwe wengine wadogo wanaoendana na kasi ya mpira wa kisasa, timu yetu ni nzuri makipa poor, beki mbili za kati poor. Uwazi unatakiwa sana katika mpira wa sasa tusikariri majina. Bado naipenda timu yangu ya taifa, nidhamu pia somo kubwa sana tumepewa kadi kizembe sana", ameandika machupa kwenye account yake ya facebook.

"Haina haja ya kupanic, tufanye marekebisho kwenye position zenye matatizo. Nimeduwaa na nimeumia sana ila hatuna jinsi, tuwape nafasi wengine Cannavaro na Yondani hawaendani na kasi ya vijana wengine".

"Mabadiliko ya mfumo wa soka letu uangaliwe pia. Kocha apewe muda, mabadiliko yanaonekana. Nimeumia na kipigo niko pamoja na timu yangu, naipenda sana Tanzania", machupa alimaliza.



Comments