LUKE SHAW AWASHUKURU MASHABIKI WA PSV KWA KUMSAPOTI



LUKE SHAW AWASHUKURU MASHABIKI WA PSV KWA KUMSAPOTI

Luke Shaw 5

Kuelekea katika mchezo wa jana usiku kati ya Manchester United na PSV Eindhoven ya Uholanzi, mashabiki wa PSV wameonesha hisia zao kwa mchezaji Luke Shaw (20) kwa kuandika mabango ya kumtakia apone haraka baada ya kuvunjika mguu mwezi September mwaka huku alipokua akicheza mechi dhidi ya PSV.

2C5A162700000578-3235800-Manchester_United_defender_Luke_Shaw_holds_his_leg_after_sufferi-m-48_1442347227257

Mchezaji Hector Moreno ambaye alimuumiza Shaw anasema pamoja na kwamba mashabiki siku zote hupenda wachezaji wao kuwa aggressive wanapokua uwanjani, lakini baada ya kuumia kwa Shaw, kila mmoja alipatwa na hisia kubwa.

Tayari Hector Moreno mwenyewe alishamtembelea hospitali na kumuomba msamaha Luke Shaw, tukio ambalo linatajwa kuwa la kiunguana na uana michezo kwani ilikua ni faraja kwa Shaw.

Luke Shaw 3

Katika kuwashukuru mashabiki hao wa PSV waliokuja na mabango yao katika uwanja wa Old Trafford, Luke Shaw ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwashukuru sana mashabiki wa PSV kwa sapoti yao.

Luke Shaw 7



Comments