NYOTA wa zamani Luis Figo amemtaka kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kukifanyia marekebisho kikosi chake ambacho kimeonyesha kiwango kibovu kilichowafanya wafungwe mechi saba kati ya 12 za mwanzo wa Ligi Kuu England.
Kwa sasa kikosi hicho cha Mourinho kipo nafasi ya 16, kikiwa na pointi 11, huku kikiwa kimepoteza mechi tatu za mwisho kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za timu ya taifa.
Hadi sasa mabingwa hao watetezi wapo nyuma kwa pointi 15 dhidi ya timu zinazoongoza Ligi hiyo, Manchester City na Arsenal na hatima ya Mourinho kuendelea kuinoa klabu hiyo ya Stamford Bridge ipo shakani.
Hata hivyo, Figo ambaye amewahi kufundishwa na Mourinho, anaamini kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 anaweza kuifanya Chelsei kuzinduka.
"Nadhani maisha ya kocha ni kama haya," alisema staa huyo wa zamani na kuongeza:."Matokeo sio mazuri, lakini hutakiwi kumlaumu kocha."
Comments
Post a Comment