Gazeti la Daily Mail la nchini England limeripoti kuwa pamoja na kocha Pep Guadiola wa Bayern Munich kuhusishwa na klabu ya Manchester City, lakini vyanzo vya karibu vya mocha huyo vinasema kuwa Pep Guadiola anataka kuifundisha Manchester United.
Pep Guadiola hajaongeza mkataba hadi sasa huku mkataba wake wa sasa ukiwa unaisha mwisho wa msimu huu. Kocha huyo alisema kuwa tusubiri hadi mwezi December kujua mustakabali wa maisha yake ya Bayern Munich na wapi anaweza kwenda.
Tayari Bayern Munich inajiandaa kuziba pengo la kocha huyo kama akiondoka. Mwenyekiti mtendaji wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenige alikaririwa wiki iliyopita akisema kuwa Bayern ni klabu kubwa na kwamba hakuna pengo lisilozibika.
Wakala wa kocha huyo alikua nchini England, Alhamis na Ijumaa za wiki iliyopita huku kukizidi taarifa za kwamba huenda wakawa wanakamilisha dili la kocha huyo kutua Manchester City.
Pep Guadiola amekua tangu awali akihusishwa na kuwa na mahaba na klabu ya Manchester United, hasa kutokana na mahusiano yake mazuri na aliyekua mocha wa klabu ya Manchester United, Sir Alex Ferguson na kwamba lolote linaweza kutokea.
Comments
Post a Comment