Inawezekana labda tukamuona Lionel Messi kwenye mechi ya El Clasico kati ya Barcelona Vs Real Madrid siku ya Jumamosi. Watu wengi walikua wanalalamika kwamba kama Messi asipokuwepo kwenye mechi hiyo basi haitakamilika kuwa El Clasico.
Hivi leo kwenye mkutano na waandishi wa habari kocha wa Barcelona B Gerard Lopez amesema kwamba leo hii Messi amefanya mazoezi na kikosi B cha Barcelona.
"Messi amefanya mazoezi leo, nimeuona akiwa vizuri na nina furaha kuona matibabu yake kuonekana yamekamilika. Namuona yupo vizuri kama tulivyomzoea", alisema kocha huyo.
"Messi alienda sawa na mazoezi yote tuliyofanya na alikua kama mchezaji wa kawaida kuanzia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo hadi uwanjani. Kwa jinsi nilivyomuona anaonekana yupo fit ila sijui kama atacheza kwenye mechi ya jumamosi ambao ni uamuzi wa kocha wake."
El Clasico itaonekana live kupitia Azam TV siku ya jumamosi saa 2:15 usiku. Haina kuadhithiwa hii kila mtu atacheki mechi kupitia Azam TV burudani nyumbani.
Comments
Post a Comment