Wakati Lionel Messi atakaporudi dimbani kutoka kwenye majeruhi katika mechi ya EL Clasico – kuna uwezekano akiwa anatokea benchi – then ile safu ya ushambuliaji ya Barcelona inayotajwa kuwa zaidi itaungana tena. Mshindi wa mara 4 wa tuzo ya Ballon d'Or anarejea kuungana na washambuliaji wenzake Luis Suarez na Neymar – ambao wote kwa pamoja waliunda safu ya ushambuliaji iliyovunja ngome zote za ulinzi za wapinzani msimu uliopita.
Ushindi wa kombe la Ulaya msimu uliopita – ulikuwa ni wanne katika kipindi cha miaka 9 – na katika mafanikio haya yote Messi amehusika.
Hapa sasa tuangalie namna safu ya ushambuliaji ya Barca ya sasa inavyoshabiiana au kutofautiana na safu nyingine za ushambuliaji za Barca ambazo zilinyanyasa sana safu za ulinzi huko Spain na barani ulaya kiujumla……
2005-07: Ronaldinho (magoli 50 katika mechi 94), Samuel Eto'o (magoli 47 katika 75), Lionel Messi (magoli 25 katika mechi 61). Jumla: Magoli 122 katika mechi 230 (Wastani wa 0.53 kwa mechi).
Frank Rijkaard aliipa Barcelona ubingwa wao wa pili wa ulaya, tangu walipopata kombe hilo mwaka 1992, pia akawawezesha kushinda kombe la La Liga msimu wa 2005-06 season.
Mpaka kufikia wakati huo Barca walikuwa wanaumudu vilivyo mfumo wa 4-3-3 – huku staa wa kikoso Ronaldinho akiwa kwenye ubora wake – akiungana na kikosi cha Barca kilichoundwa vyema na kocha aliyeondoka kabla hajawasili Camp Nou – Louis van Gaal, pia aliunda Messi nae ndio alikuwa akiibukia kwenye soka la kiwango cha dunia.
Messi aliachwa nje ya kikosi cha kwanza cha fainali ya Champions League 2006 na kumpisha winga wa kifaransa Ludovic Giuly, lakini kabla kiwango cha Ronaldinho hakijaanza kushuka, safu hii ya ushambuliaji ndio ilikuwa inatisha zaidi barani ulaya.
2007-09: Thierry Henry (magoli 45 katika mechi 89), Samuel Eto'o (53 magoli katika mechi 81), Lionel Messi (Magoli 54 katika mechi 91). Jumla: Magoli 152 katika mechi 261 (Wastani wa 0.58 kwa mechi).
Ronaldinho alipata mbdala mpya – mfungaji bora wa muda wote wa Arsenal Thierry Henry katika safu ya ushambuliaji – huku mbrazil akianzia benchi au akirudi kucheza kwenye safu ya kiungo kabla ya kuhamia AC Milan mnamo July 2008.
Mtu mwingine aliyeondoka msimu huo baada ya misimu miwili ya bila kombe la lolote – alikiwa ni kocha Frank Rijkaard, ambaye mbadala wake alikuwa kocha mdogo kiumri bila uzoefu wowote wa ukocha katika ngazi ya juu – Pep Guardiola.
Katika msimu wake wa kwanza, Guardiola alibeba makombe yote, akishinda 'treble' kwa kumuhamishia Messi katika nafasi ya ushambuliaji katikati, akiwa na usaidizi aa Eto'o na Henry.
Msimu wa 2010-11: David Villa (Magoli 23 katika mechi 52), Lionel Messi (Magoli 53 katika mechi 55), Pedro (Magoli 22 katika mechi 53). Jumla: Magoli 98 katika mechi 160 (Wastani wa 0.61 kwa mechi).
Mwanzoni mwa msimu wa 2010-11 wote wawili Henry na Eto'o walikuwa wameshaondoka, Zlatan Ibrahimovic, akaingia kikosini na kudumu Catalonia kwa msimu mmoja baada ya kushindwa kuelewana na Messi na Guardiola.
Barca bado walishinda La Liga na Zlatan akafunga magoli 21 katika mashindano yote lakini takwimu hizi zilionyesha kufeli.
Ujio mpya wa washambuliaji wakawa ni wahispania Villa na Pedro – Villa akitokea Valencia na Pedro akitokea kwenye academy ya Barca – hawa walimsaidia sana Messi katika kukuza kipaji chake.
Watatu hawa watakumbukwa walivyoiharibu safu ya ulinzi ya Manchester United katika fainali ya Champions League 2011 lakini baadae kidogo wawili hao wakapoteza nafasi zao kwa Alexis Sanchez na Cesc Fabregas – Villa akahama na Pedro akawa anatokea benchi.
2014- : Neymar (Magoli 52 katika mechi 66), Luis Suarez (Magoli 25 katika mechi 43), Lionel Messi (Magoli 64 katika mechi 66). Jumla ni magoli 141 katika mechi 175 (Wastani wa 0.81).
Huku wakiwa wameshinda kombe moja tu la La Liga na moja la Copa del Rey katika kipindi cha miaka mitatu, Barca wakacheza kamari ya kumsajili Suarez mwaka 2014 pamoja na kwamba alikuwa kafungiwa mpaka October baada ya kumng'ata Giorgio Chiellini kwenye World Cup.
Neymar alionyesha uwezo wake mkubwa katika msimu wake wa kwanza lakini akisaidiwa na Fabregas na Sanchez hakuweza kuunda ushirikiano mzuri na Messi kama ambavyo ilivyokuwa safu ya ushambuliaji ya miaka 2006, 2009 au 2011.
Kuwasili kwa Suarez kuliongezea ubora safu ya ushambuliaji iliyopo na kuwaunganisha vyema Messi na Neymar na watatu hawa wakavunja rekodi za ufungaji msimu uliopita katika msimu ambao Barca chini Luis Enrique walishinda 'treble'.
Pamoja na kucheza kwa msimu mmoja tu – Safu hii ya ushambuliaji ina wastani mkubwa wa kufunga kuliko safu nyingine yoyote katika miaka ya hivi karibuni – na kuelekea kwenye El Clasico kesho watatu hawa watakuwa wanacheza pamoja baada ya miezi kadhaa sasa.
Comments
Post a Comment