KOCHA DIEGO SIMEONE SASA AHUSISHWA NA CHELSEA




Diego Simeone believes            his side are back on track after failing to retain their La            Liga title last season
KLABU ya Chelsea inamfuatilia kwa karibu Diego Simeone ili kurithi mikoba ya Mreno Jose Mourinho, wakati huu ambao Muargentina huyo anaangalia jinsi ya kuondoka Atletico, Madrid mwishoni mwa msimu.

Mbali na kocha huyo, Chelsea pia inawafikiria kocha wa zamani wa Liverpool, Brendan Rodgers, Roberto Di Matteo na Guus Hiddink.

Uamuzi huo umekuja ikiwa ni baada ya Chelsea kudorora msimu huu, ikiwa imepoteza mechi saba kati ya 12 za Ligi Kuu England, ikishinda tatu ytu na kupata sare mbili.

Hali hiyo imewafanya kuwa katika nafasi ya 16 baada ya kujikusanyia pointi 11 ndani ya mechi 12, huku Manchester City ikiwa kileleni na pointi zao 25, sawa na Arsenal na Leicester City zinazotofautiana kwa mabao.


Comments