KOCHA BRAZIL MAPIGA CHAPUO NEYMAR KUWAPIKU MESSI NA RONALDO


KOCHA BRAZIL MAPIGA CHAPUO NEYMAR KUWAPIKU MESSI NA RONALDO

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Dunga amemuonya nahodha wake, Neymar Jr akimtaka kuongeza bidii uwanjani ili awapiku Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Dunga alisema jna kwamba, imefika wakati kwa mchezaji huyo wa Brazil kuonyesha kwamba ana uwezo mkubwa kuliko nyota hao.

Alisema, ana imani uwezo wa Neymar ni mkubwa sana kama ataongeza bidii ya kufanya mazoezi na kujifunza mambo zaidi kutoka kwa Ronaldo na Messi.

"Hawa ni wachezaji wazuri, lakini bado nina imani kwamba anatakiwa kuongeza bidii ya kutosha ili aweze kufunga mabao zaidi," alisema.


Comments