KIPOBA WA CHELSEA ROMAN ABRAMOVIC YUPO TAYARI KUVUNJA BENKI KWAAJILI YA LIONEL MESSI



KIPOBA WA CHELSEA ROMAN ABRAMOVIC YUPO TAYARI KUVUNJA BENKI KWAAJILI YA LIONEL MESSI
BILIONEA mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovic amezisikia tarifa njema zinazomhusisha straika kinara wa Barcelona, Leonel Messi kutua katika kikosi cha The Blue, ambapo amesema kama anahitajika kweli yuko tayari kuvunja benki kwa ajili ya staa huyo raia wa Argentina.

"Mambo yakienda sawa, fedha sio tatizo kwa ajili ya mchezaji bora kama huyu. Ana manufaa mengi kisoka na kibiashara kuliko gharama zinazohitajika," alinukuliwa Abramovic.

Juma moja sasa kumekuwapo kwa taarifa za Messi kutaka kutua katika kikosi cha Jose Mourinho, lakini mara kadhaa uvumi huo umekuwa ukikanushwa na pande zote mbili.

Lakini safari hii, uvumi huu umemfikia kibopa mwenyewe wa Chelsea na amekaririwa akisema kuwa atawajibika kwa lolote litalohusu kinara huyo wa kupachika mabao ndani ya Barca.

Akinukuliwa, Abramovic amesema kila jambo linawezekana chini ya jua na kwamba Messi ni kati ya nyota bora duniani, hivyo si tarifa za kupuuzwa.

Alisema, amezisikia taarifa hizo juu juu na atasubiri kusikia ukweli kutoka kwa meneja wa kikosi chake, Jose Morinho.

"Kuhusu Messi kujiunga Chelsea FC ni habari njema lakini zinahitaji ufuatiliaji na uthibitisho sahihi kutoka pande zote mbili."


"Ukweli utabaki kuwa kweli siku ya mwisho, lakini suala la fedha si tatizo kwasababu ni jambo linalowezekana katika mazungumzo," alinukuliwa kibopa huyo mwenye mkwanja wa kutosha.  


Comments