KAMA ULIKUWA UNADHANI HAZARD ANA BIFU NA MOURINHO SOMA HAPA


KAMA ULIKUWA UNADHANI HAZARD ANA BIFU NA MOURINHO SOMA HAPA
Eden Hazard is still a            target for the opposition despite his manager Jose Mourinho            asking for more protection
PAMOJA na shutuma zinazomkabili kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kutokana na mwenendo usioridhisha, staa wa timu hiyo, Eden Hazard ametamka hadharani kuwa hakuna kocha bora na anayefaa kuiongoza klabu hiyo ya jijini London zaidi ya raia huyo wa Ureno.

Chelsea ilizinduka kwenye Premier League wikiendi iliyopita kwa kuichapa Norwich bao 1-0 ndani ya  dimba la Stamford Bridge, baada ya kuambulia kipigo katika michezo mitatu iliyopita.

Kauli ya nyota huyo inakuja baada ya shutuma za hivi karibuni kuwa kiwango chake kimeporomoka kutokana na kutoelewana na Mourinho lakini straika huyo amekanusha vikali uvumi huo.

"Nimesikia maneno mengi kuhusu mimi kuwa na matatizo na kocha Mourinho, lakini si kweli," alisema mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita, tuzo inayotolewa na chama cha wachezaji wa kulipwa nchini England.

"Hakuna ugomvi kati yetu. Ni kocha bora kwa Chelsea na tutashinda mataji mengi tukiwa pamoja. Inawezekana isiwe msimu huu, lakini si msimu ujao na inayofuata," alisema.


Comments