KAMA ULIKUWA HUJUI, JANA POGBA ALIVAA VIATU MAALUMU VYENYE UJUMBE KUHUSU SHAMBULIO LA KIGAIDI UFARANSA



KAMA ULIKUWA HUJUI, JANA POGBA ALIVAA VIATU MAALUMU VYENYE UJUMBE KUHUSU SHAMBULIO LA KIGAIDI UFARANSA

Pogba 1

Kiungo Paul Pogba jana usiku alionesha uzalendo kwa taifa lake baada ya kuvalia viatu maalumu vyenye rangi ya bendera ya Ufaransa akiiongoza Juventus kuwafunga Manchester City goli 1-0 katika kuwaenzi wahanga wa mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika Paris Juma lililopita.

Paul Pogba alikuwepo uwanjani wakati magaidi wanafanya mashambulizi nje ya uwanja wa Stade de France wiki iliyopita huku watu wasiopungua 130 wakipoteza maisha.

Pogba

Katika mchezo wa jana dhidi ya Manchester City, Paul Pogba alikua kiungo muhimu huku akiizidi safu ya kiungo ya City chini ya Yaya Toure na wenzake huku akihusika katika kutengeneza goli lililofungwa na mshambuliaji Mario Mandzukic.

Baada ya ushindi huo, Juve imejikita kileleni mwa kundi hilo na kuiacha City katika nafasi ya 2 kila timu ikibakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Pogba 2



Comments