ZOEZI la uwekaji nyasi bandia kwenye uwanja wa Kaitaba uliopo mjini Bukoba, limekamilika na sasa upo tayari kutumika kwa mechi za Ligi Kuu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa chama cha soka mkoa Kagera, ni kwamba uwanja huo utaanza rasmi kutumika kwenye mzunguuko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kukamilika kwa uwanja huo ni ukombozi mkubwa kwa wana Kagera wote na pia wanaamini kutaiwezesha timu ya Kagera Sugar kufanya vema.
Inaaminika Kagera Sugar ambayo ilianza kuutumia uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuhamia Kambarage mjini Shinyanga na hivi sasa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, imeathirika sana kwa kukosa sapoti ya mashabiki wake.

Comments
Post a Comment