JURGEN KLOPP APIGANIA NAFASI YA KUCHEZA CHAMPIONS LEAGUE LIVERPOOL



JURGEN KLOPP APIGANIA NAFASI YA KUCHEZA CHAMPIONS LEAGUE LIVERPOOL
Lijnders (right) watched Liverpool's Under 18s alongside            Klopp (left) shortly after he was appointed manager
Licha ya kwamba bado hana rekodi za kujivunia tangu alipoanza kuikochi Liverpool,  kocha Jurgen Klopp amejitapa kwamba muda wa kuibeza timu hiyo umemalizika na sasa ni wakati wa kushuhudia mambo mazuri.
Mjerumani huyo aliyetua Anfield kuchukua nafasi ya Brendan Rodgers, amesema atahakikisha timu hiyo inapigania kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hapo mwakani.
 "Wakati mwingine tunatakiwa kucheza mechi saba ndani ya mwezi mmoja, ni jambo gumu lakini tunapambana kwa nia ya kushinda," alisema.
Alisisitiza kuwa, hakutakuwa na mapumziko kwa wachezaji wake wakati wa sikukuu na kwamba anataka kuona wachezaji wote wanapigania nafasi na sio kukaa benchi.


Comments