MWANAUME ameanza kazi. Kama mtu ulikuwa hujui vurugu zake, sasa unaweza kumtambua Jurgen Klopp, kocha wa Liverpool ya Uingereza.
Jana Jumamosi Klopp amekaririwa akisema kwamba ameshatenga kiasi cha euro mil. 25.4 kwa ajili ya kumnyakua winga machachari wa FC Barcelona ya Hispania, Cristian Tello.
Kocha huyo amesema kwamba ana uhakika katika dirisha la usajili la mwezi januari, mchezai huyo atakuwa sehemu ya Liverpool na ndie atakuwa ameziba kwa uhakika kabisa pengo la Raheem sterling ambaye amehamia Manchester City.
Mazungumzo kati ya Jurgen Klopp na kinda huyo wa Hispania yanadaiwa kwamba yamefikia mahali pazuri na inasemekana kuwa Barceona hawana hiyana kumwachia nyota huyo.
Gazeti la michezo la Metro limeandika kwamba uwezekano wa Barcelona kumwachia Cristian Tello ni mkubwa kwa sababu tayari mchezaji huyo kwa sasa anacheza kwa mkopo katika kikosi cha FC Porto ya Ureno.
Klopp tayari ameshaomba pesa hizo kwa uongozi wa Liverpool na kwamba ameambiwa akitaka kiasi chochote cha pesa atapewa ili kusajili nyota anayemhitaji.
Nyota huyo wa miaka 24 alikuwa anaisaidia sana Barceona katika Primeira Liga katika michezo mbalimbali aliyocheza na ameifungia mabao 10 na kusaidia kupatikana kwa mabao mengine 12.
Kocha huyo amesema kwamba anataka kuhakikisha mchezaji huyo anajiunga na Liverpool ili kuimarisha winga yake ya kulia ambayo imekuwa haina makali toka kuondoka kwa Sterling.

Comments
Post a Comment