KOCHA mkuu wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amekiri wazi kuwa atakuwa anadanganya kama wafanyavyo wasanii wa maigizo ikiwa atasema kikosi chake kitaibuka na ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
Hata hivyo Mourinho amesema licha ya kupoteza imani ya kutetea taji, lakini bado hajakata tamaa ya kumaliza mbio za ubingwa huo akiwa 'top four'.
Kauli ya kocha huyo inakuja baada ya mwishoni mwa wiki timu yake kuichapa Norwich bao 1-0 kupitia kwa straika Diego Costa ambapo Mourinho alikataa kuwa ushindi huo ndio mwanzo wa kutetea ubingwa wa Premier League.
"Kumaliza katika nafasi nne za juu ni jambo linalowezekana kwangu. Utakaponiuliza kuhusu kuchukua ubingwa nitakwambia kuwa haiwezekani, labda Tom Cruise (mwigizaji wa Marekani) anaweza kufanikisha hilo. Nafasi ya nne ni ngumu kuipata lakini inawezekana," alisema Mourinho.
"Ushindi huu unatia moyo. Tulikuwa na presha. Tulihisi hilo lakini tuliendana na hali hiyo na tukafanikiwa kupata matokeo tuliyoyahitaji sana," aliongeza kocha huyo mwenye maneno mengi.
Comments
Post a Comment