JOSE MOURINHO AANZISHA VITA MPYA NA ARSENE WENGER ...asema anatamani Arsenal ing'olewe Champions League
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho ameanzisha vita mpya ya maneno dhidi ya Arsene Wenger, baada ya kukiri hadharani kuwa anataka Arsenal itolewe Ligi ya Mabingwa Ulaya.
The Gunners walijipa uhai katika michuano hiyo, baada ya juzi kuifunga Dinamo Zagreb.
Kikosi hicho cha Wenger bado kinaweza kutinga hatua ya mtoano iwapo kitaifunga Olympiakos kwa magoli 2-0 mjini Athens, au kufikia ushindi wa 3-2 Wagiriki hao waliopata wakiwa Emirates.
Lakini Mourinho baada ya kuiona Chelsea ikiendelea kushamiri katika michuano hiyo baada ya kushinda 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv, anatumai Wagiriki hao watakuwa pigo kwa Wenger.
Akisisitiza kuwa, si rahisi kwa Arsenal kusonga mbele, bosi huyo wa Chelsea alibainisha atakwenda kinyume na Arsenal.
Alisema "Arsenal wapo kwenye kundi ambalo rafiki yangu mtoto Marco Silva ni meneja wa Olympiakos.
"Itapendeza Marco akifanikiwa kuendelea hatua nyingine, nataka kuwa wazi kabisa na nasema ningependea Olympiakos iendelee."
Comments
Post a Comment