Mchezaji na mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy amevunja rekodi ya kuwa mshambuliaji aliyefunga magoli mengi zaidi na katika mechi nyingi mfululizo.
Jamie Vardy kavunja rekodi ya Ruud Van Nistelrooy baada ya kufunga goli katika mechi 11 mfululizo. Goli la kufikisha safari ya mechi 11 mfululizo akifunga limekuwa dhidi ya timu ya zamani ya Nistelrooy yaani Manchester United akifunga katika kipindi cha kwanza.
Mchezaji Ruud Van Nistelrooy aliweka rekodi ya awali kwa michezo ya misimu miwili ya mwaka 2003. Mpaka anavunja rekodi hii Vardy amefunga magoli 13 katika kipinid hiki huku pia akiwa amefunga magoli 14 na kuongoza orodha ya wafungaji ligi kuu ya Uingereza.
IFAHAMU SAFARI YA UFUNGAJI WAKE KATIKA MECHI HIZI 11
29 August: Bournemouth 1-1 Leicester
13 September: Leicester 3-2 Aston Villa
19 September: Stoke 2-2 Leicester
26 September: Leicester 2-5 Arsenal
3 October: Norwich 1-2 Leicester
17 October: Southampton 2-2 Leicester
24 October: Leicester 1-0 Crystal Palace
31 October: West Brom 2-3 Leicester
7 November: Leicester 2-1 Watford
21 November: Newcastle 0-3 Leicester
28 November: Leicester v Manchester United
VIDEO YA GOLI LA 11 LA VARDY
Comments
Post a Comment